I made a harambee for my school fees and got Kshs.700 bob

Ilifaa nijoin 2023/2024 but sikuweza sababu ya ukosefu wa karo. Mamangu hawezi membea vizuri sababu ya stroke na pia babangu amekuwa mzee na hana kazi ya kuweza kunilipia karo. Nilipata 331 in KCPE and B plain, 61 points in KCSE. Tulizaliwa wanne lakini wote watatu washafariki ni mimi tu, ambaye ni last born,nimebaki.

     

Niliitwa Kenyatta University, but niliweza kudefer nikifikiria mwaka huu ungekuwa sawa. Nimejaribu kuwafikia viongozi wetu, kama area MP lakini nimezungushwa hadi ile pesa kidogo nilikuwa nayo imeishia transport.

Nilijaribu kufikia area MCA lakini aliniambia niunde Whatsapp group nim-add. Nilifanya hivyo, watu wakaingia. Wengi wani-pledge tu hadi MCA ambaye aliniambia niunde, tangu apledge, sijaweza kumpata kwa simu. Zimebaki wiki mbili nireport shule lakini sioni dalili sababu so far, niko na Ksh. 700 bob tu ambayo nilipata kupita hiyo group. Wengi walileft