Nikiwa shughuli zangu nilikutana na huyu mtoto na juu nilikua nahisi njaa, nikaamua kununua mahindi ambayo alikua anauza. Nilikaribia na baada ya kumuuliza bei akaniambia. Katika harakati ya kunifungia ndo nikagundua kumbe ni mtoto mdogo. Nikaamua kumuuliza maswali kidogo na hivi ndo alinijibu.



“Mama ndo amekua akinilipia school fees tangu nianze shule, amekua akiuza bagia, kama Sahi nimemwacha nyumbani akiuza bagia nami nikakuja kuuza mahindi. Mimi ndiye tu mtoto wa kipekee kwetu sina dada wala kaka, ni Mimi tu. Baba naye amezikwa tu juzi, only 5 days ago ndo mazishi ilifanywa na sasa tuko tu mimi pamoja na mama yangu mzazi. “
This really hit me deeply. Hapo nilimuuliza bei ya mahindi yote alikua nayo akaniambia ni Ksh 320 pekee. Nilitoa 2k nikampa na nikamwomba namba ya mama. Nilipopiga nilipata iko off, nikaambia mtoto aambie mamake akipata missed call anipigie, kisha nikamwambia arudi nyumbani. This is so heartbreaking.
Remember to support Our Makanda Foundation the number is 0713481436 (Phelix Joel) .