He Defil£d My 2yr-old baby and Still Threatens To K¡ll Me

He Defil£d My 2yr-old baby and Still Threatens To K¡ll Me, ????

Ni kama kuna game nimechezwa sababu sina wa kunishika mkono. I’m a single mom of 4. Najaribu sana ili nione watoto wangu wako sawa sababu sina kazi ama biashara, nafulia watu tu. Niko na mmoja yuko form 1, mwengine class 8, lower class and the last born 2yrs.

Sijakuwa na amani tangu mtoto wangu afanyiwe unyama. Nilimpeleka hospitalini ili afanyie matibabu, ashonwe lakini niliitishwa pesa zenye sikuweza kufikia. Niliambiwa kuna aina nyingi za test, zingine 5K, zingine 10K ndivyo nije ninunue dawa nje.

Sikuweza kufikia hiyo yote. Nilikopa pesa kidogo akafanyiwa test moja tu kisha nikapewa dawa ya kumuoshea tu lakini hakuna dalili. Mtoto hajapona na harufu inatoka vibaya yenye inanishtua sana sababu labda aliumizwa hadi ndani sana ????

I reported the case, the guy was arrested and after that the rest is drama. Naambiwa kuwa alipelekwa kotini, ambayo sikuambiwa alipelekwa lini, mara naambiwa alitoka kwa bond.

Tangu siku hiyo, maisha yangu haijakuwa sawa sababu familia ya huyo jamaa inanifuata sana. I’ve reported the matter, I have more than 4 OBs of threats but nothing has happened.

Nagongewa mlango kila usiku kwa vitisho. Kuhama siwezi sababu sina hata pesa ya kutafuta nyumba nyingine mbali na hapa. Hata ya dawa imenishinda na mtoto anazidi kuumia na kutoa uzaha! ????

Bibi yake amewahi kuja hapa akanitishia kuwa wataniuwa nisipoachana na kesi hiyo, sina la kufanya sababu hata mimi sielewi vile kesi hiyo inaenda. Dawa imenishibda kupata, kuhama siwezi, vyakula ni shida na rent arrears ni 3 months. Nimechoka! ???? ????