Katika mahojiano yangu na Shosh aliniambia mambo mengi na shida alizokua anakumbana nazo. Nilijaribu kuangalia nyumba nikaona iko karibu kuanguka na hapo kwa nilimuahidi kuwa Foundation yetu ambayo inaitwa Makanda Foundation tungemjengea nyumba mpya ambayo angekaa pamoja na msichana wake. Katika baadhi ya mahojiano yangu na yeye haya ndo alikua nayo ya kusema. ““Maisha yangu nimemuachia Mungu tu. Naweza enda saa yoyote sababu sijui nyumba itanianguakia saa ngapi nikilala. Mvuani nyingi, upepo kila saa,Nilibakisha watoto wawili baada ya kuzika wengine. Mmoja ni mlemavi, mimi ndiye kila kitu kwake, yuko tu kwa nyumva. Wa pili, ni msicha wangu huyu, nimemuuguza karibu mwaka unaisha. Sina mtu yeyote wa kunisaidia sababu wale ambao wangenisaidia sasa wako kwa Mungu. ???? Siwezi kupalilia vizuri sababu ni mimi tu mtu mmoja, sina pesa ya mbegu na mbolea. Nang’ang’ana kupata hata ya chakula,Kula kwetu ni bahati sababu nisipopata, tunalala hivyo…”
Ahadi ambayo nilimpa tayari nishatimiza kwa kupitia Makanda Foundation pamoja na Wasamaria Wema nimemjengea nyumba mpya. Mungu siku zote. On the Next one.Kumbuka kwa kusupport Our Makanda Foundation number ni 0713481436 (phelix Joel).